Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mitoko ya Man United bila Hojlund

Rasmus Hojlund EPL Statistics Rasmus Hojlund

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Majeraha ya straika Rasmus Hojlund ni pigo kubwa kwa Manchester United na kumwacha Kocha Erik ten Hag njiapanda.

Straika huyo alipata maumivu ya misuli ambayo yanaweza kumweka nje ya uwanja kwa wiki mbili hadi tatu.

Atakosa mechi dhidi ya Nottingham Forest kwenye Kombe la FA na ile ya Ligi Kuu England ya Manchester Derby, dhidi ya mahasimu wao Manchester City mwezi ujao.

Man United inamkosa pia Anthony Martial kutokana na kuwa majeruhi na hilo linamfanya kocha Ten Hag kuwa na machaguo machache kwenye safu yake ya ushambuliaji.

Majeraha ya Luke Shaw na Aaron Wan-Bissaka ina maana Man United itahitaji kufanya mabadiliko kwenye safu yao ya mabeki na Victor Lindelof alitarajia kutumika kwenye nafasi ya Shaw kwenye mechi ya Aston Villa na Luton. Lakini, kuna machaguo machache sana kwa Ten Hag kwa kukosekana Hojlund.

Chaguo la Kwanza; Marcus Rashford kucheza kwenye nafasi ya mshambuliaji wa kati kama ambavyo amejaribiwa kucheza hivyo mara kadhaa.

Rashford ana kasi na uwezo mkubwa wa kufunga kama Hojlund. Lakini, kwa kitendo cha kumtumia winga huyo kama mshambuliaji wa kati, hapo Antony italazimika kuanza, huku chaguo jingine linaweza kuwa Amad Diallo.

Chaguo la Pili; Kocha Ten Hag anaweza kubaki na Rashford na Alejandro Garnacho kwenye wingi kama ambavyo amekuwa akiwatumia kwa siku za karibuni na timu kushinda.

Lakini, kutokana na kutokuwa na straika ambao yupo fiti, basi kwenye eneo hilo la mshambuliaji wa kati anaweza kuanza na Amad Diallo.

Chaguo la Tatu; Kama Ten Hag ataona Diallo hayupo tayari, basi anaweza kumtumia mfungaji bora namba mbili wa Man United msimu huu, Scott McTominay.

Staa huyo wa kimataifa wa Scotland hajawahi kucheza nafasi ya mshambuliaji wa kati tangu utoto wake, lakini anafahamu namna ya kufunga mabao na hadi sasa msimu huu ameshafunga mara nane kwenye michuano yote. Kimo chake kinaweza kuwa na faida, akipangwa kwenye nafasi ya mshambuliaji wa kati na kusubiri krosi za Rashford na Garnacho.

Chanzo: Mwanaspoti