Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mitaa haiwezi kumsahau Antonio Di Natale

Di Natale Antonio Di Natale

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni kwa sababu Alessandro Del Piero alicheza Juventus. Jina lake likaimbwa kila mahala katika Ulimwengu wa Soka.

Ni kwa sababu Roberto Baggio amecheza Juventus na Inter. Jina lake utalikuta katika kumbukumbu maarufu za wapenda Soka.

Ni kwa sababu Francesco Totti amecheza AS Roma. anapewa heshima yake inayostahili.

Ndio maana mnawaimba

Ila

Kuna balaa la huyu kiumbe ambaye aliapa mbele ya Rais wa Udinese Giampaolo Pozzo kwamba atacheza Udinese Calcio mpaka miguu yake itakapoisha nguvu.

Chuma kimezaliwa Naples lakini hakikutaka kusikia hadithi za kwenda Napoli, sembuse Juventus?

Wengi tumenunua magazeti kipindi hicho then tunaingia kwenye orodha za wafungaji bora wa ligi ya Serie A, hulikosi jina la mhuni Antonio Di Natale.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live