Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Misri yaanza kampeni ya kufuzu kombe la dunia kwa kishindo

Mo Salah 2 Misri yaanza kampeni ya kufuzu kombe la dunia kwa kishindo

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mohamed Salah alifunga mabao manne na kuandika rekodi mpya ya ufungaji kwenye Timu yake kwa Misri wakati wa mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Djibouti huku Nigeria wakilazimishwa sare na Lesotho, jana Alhamisi.

Salah aliihakikishia Misri ushindi wa mabao 6-0 katika mechi yao ya ufunguzi ya Kundi A mjini Cairo huku mshambuliaji huyo akitupia mabao manne ya kwanza na kuongeza jumla ya mabao yake kwa Misri hadi 53 katika mechi 93 huku wakitafuta nafasi ya kutinga fainali za 2026, wakiwa na alikosa Kombe la Dunia la Qatar mwaka jana.

Raundi mbili za kwanza za mchujo wa Afrika zitachezwa kuanzia Jumatano hadi Jumanne ijayo, na zitaendelea Juni mwakani.

Kuna makundi tisa ambapo mshindi anafuzu kwa fainali za 2026 nchini Canada, Mexico na Marekani lakini washindi wanne bora wanapata nafasi zaidi ya kufuzu kupitia mfumo wa awamu mbili za mchujo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live