Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Misri kufa au kupona, ikiisaka 16 bora bila Salah

Salah AFCON Misri kufa au kupona, ikiisaka 16 bora bila Salah

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mabingwa mara saba wa fainali za Mataifa ya Afrika, Misri watacheza mechi ya kufa au kupona leo dhidi ya vinara Equitorial Guinea, ili kusonga mbele hatua ya 16-Bora.

Equitorial Guinea imefuzu hatua ya 16-Bora baada kushinda mechi zote mbili za kwanza ikionyesha kiwango kilichomshangaza kila mmoja na leo itacheza mechi ya kukamilisha ratiba dhidi ya Mafarao wa Misri baada ya kujihakikishia kumaliza kileleni ikiwa na pointi 6.

Timu zote tatu zilizobaki katika kundi hilo, Misri yenye pointi 2, Ghana (1) na Msumbiji (1), kila moja ina nafasi ya kufuzu kwa kutegemea matokeo ya mechi zao za mwisho ambazo zitachezwa muda mmoja leo saa 5:00 usiku.

Hata hivyo, kama mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo, Misri watashinda dhidi ya Equitorial Guinea, Mafarao hao watafuzu moja kwa moja kwa sababu watafikisha pointi 5, na kuzivurugia Ghana na Msumbiji, ambazo mojawapo ikiifunga nyingine itaishia kufikisha pointi 4, ambazo ili kufuzu itategemea na nafasi mbili za ‘best looser’ kwa timu zenye matokeo bora miongoni mwa makundi sita ya michuano hiyo ya 34 ya Afcon.

Misri inatarajia kumkosa supastaa wake kutoka katika klabu ya Liverpool ya Ligi Kuu ya England, Mohamed Salah, ambaye aliumia misuli dhidi ya Ghana na anatarajiwa kukosa mechi mbili.

Wababe hao hawajawa na michuano mizuri wakilazimisha sare kwa penalti ya dakika ya mwisho iliyofungwa na Mo Salah dhidi ya Msumbiji wakitoka 2-2 katika mechi yao ya ufunguzi na kisha kulazimisha sare ya 2-2 tena dhidi ya Ghana, ambayo mabao yote ya The Black Stars yalifungwa na Mohamed Kudus wa West Ham United ya Ligi Kuu England. Ratiba za leo moto utawaka.

Chanzo: Mwanaspoti