Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Misri, Ghana hakuna aliye salama

Afcon Egypt Vs Ghana Misri, Ghana hakuna aliye salama

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ghana na Misri kila moja inakabiliwa na presha kubwa ya kuhitaji ushindi huku ikiombea mabaya kwa mwenzake ili kujihakikishia tiketi ya kutinga hatua ya 16 bora kupitia kundi B wakati zitakapokuwa uwanjani katika viwanja tofauti leo.

Miamba hiyo miwili ya soka barani Afrika, inapiganianafasi moja ya kufuzu hatua inayofuata ya mashindano ya Afcon baada ya Cape Verde kuwa ya kwanza kufanya hivyo katika kundi lao, vinginevyo mojawapo italazimika kutegemea nafasi mojawapo kati ya nne za timu shindwa zenye matokeo bora katika makundi.

Katika Uwanja wa Allasane Ouattara, Abidjan, Ghana itakabiliana na Msumbiji ambapo ikiibuka na ushindi itafikisha pointi nne ambazo zitaifanya itinge moja kwa moja hatua ya 16 lakini hilo litatimia iwapo Misri itapoteza au kutoka sare na Cape Verde.

Maajabu ya mechi hiyo ambayo itachezwa kuanzia saa 5:00 usiku ni kwa Msumbiji inayoshika mkia ambayo nayo inaweza kufuzu kama itapata ushindi na kisha Cape Verde ikapata ushindi au kulazimisha sare na Misri iliyo na pointi mbili.

Misri yenyewe haina presha kubwa kulinganisha na Ghana kwani inahitaji ushindi tu katika mechi yake dhidi ya Cape Verde itakayochezwa katika Uwanja wa Felix Houphouet Boigny, Abidjan kuanzia saa 5:00 usiku ili ifikishe pointi tano ambazo zitaipeleka katika hatua inayofuata.

Msisimko mwingine kwa mechi za leo upo katika kundi A ambapo Guinea ya Ikweta, Ivory Coast na Nigeria kila moja ina nafasi ya kusonga mbele kutegemeana na matokeo ya mechi za leo.

Kinara wa kundi hilo, Guinea Ikweta yenye pointi nne, inahitaji ushindi au sare tu katika mechi yake dhidi ya wenyeji Ivory Coaast itakayochezwa katika Uwanja wa Allasane Ouattara kuanzia saa 2:00 usiku ili iweze kutinga hatua ya 16 bora wakati wenyeji wao watakuwa wanahitaji ushindi ingawa sare inaweza kuwabeba na kuwafanya wapite kwa nafasi nne za viti maalum.

Kwenye Uwanja wa Felix Houphouet Boigny, Nigeria inayoshika nafasi ya pili kwenye kundi hilo nayo ikiwa na pointi nne, itakabiliana na vibonde Guinea ya Ikweta ambayo tayari imeshaaga mashindano hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live