Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miquissone wa enzi zilee, ameanza kurejea

Jose Luis Miquissone JJ.jpeg Miquissone wa enzi zilee, ameanza kurejea

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchqambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka EA Radio, Ibra Kasuga amesema kuwa kiungo mshambuliaji wa Simba Sc, Luis Miquissone ameanza kurejea kwenye ubora wake alioondoka nao misimu miwili iliyopita kwenda Al Ahly.

Licha ya kuanza vibaya hapo mwanzoni, Miquissone ameonekana kuanza kuingiza kwenye mfumo wa Simba na kufanya vizuri tofauti na aliposajiliwa na timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu.

"Ukimuangalia Luis Miquissone namna ambavyo anacheza yaani yeye peke yake individually unamuona kuna zile touches ni kama vile zimerudi, hali ya kujiamini imerudi, uwezo wa ku-handle ball, namna ambavyo anauficha mpira unasema kwamba walau kuna vitu ambavyo vinakuja.

"Ukiangalia aina ya assist ama ile cross aliyoipiga kwa utulivu mkubwa, anaupiga ule mpira na Baleke anaenda kufunga unaona kabisa psychologically ameanza kukaa sawa na ameanza kurejea," amesema Ibra Kasuga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live