Luis Miquissone kiungo wa Simba taratibu anarejea kwenye makali yake kutokana na kuwa na mchango mkubwa wa upatikanaji wa mabao ndani ya timu hiyo.
Kiungo huyo sio chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Roberto Oliveira ambapo mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar alianzia benchi.
Alipopata nafasi ya kuonyesha balaa lake, alitoa pasi yake ya kwanza ya bao kwenye ligi akimpa mshikaji wake Clatous Chama aliyeuzamisha mpira mazima nyavun.
Mbali na kutoa pasi hiyo ya bao kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union uliochezwa Uwanja wa Uhuru Septemba 21 alipoanza kikosi cha kwanza alichezewa faulo ndani ya 18 dakika ya 37.
Pigo la penalti lililotolewa na mwamuzi Ahmed Arajiga ni Jean Baleke alipewa apige na Luis akakamilisha hat trick ubao uliposoma Simba 3-0 Coastal Union.
Kigongo kingine kwa Luis ambaye ana muonekano wa kibonge kwa sasa aliendeleza kwenye mchezo dhidi ya Singida Fountain Gate alipotoa pasi ya bao la ushindi kwa Moses Phiri na ubao ukasoma Singida Fountain Gate 1-2 Simba.
Oktoba 20 ni Simba v Al Ahly mchezo wa African Football League, Uwanja wa Mkapa ikiwa ni mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo ya kimataifa.