Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miquissone anarudi, aongoza kwa 'assist' Simba SC

Jose Luis Miquissone Carrier Miquissone anarudi, aongoza kwa 'assist' Simba SC

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuna namna nyingi kwenye kupima kiwango cha mchezaji, kuna kuangalia kujitoa kwa mchezaji akiwa uwanjani lakini pia unaweza kuangalia namba za huyo mchezaji kwa maana magoli ,assist muda aliocheza nk kama wengi wanavyopima siku hizi.

Kwa muda ambao Luis amekuwa akipata Simba SC chini ya Robertinho kwangu ni ngumu kusema ameanza kurudi kwenye kiwango chake lakini pia ni ngumu kusema ameisha.

Akiwa uwanjani huoni jicho la umakini kwa timu pinzani wakimtazama kama mchezaji hatari kama alivyokuwa kabla hajaondoka , lakini pia namna yake ya kulazimisha sio ile kama utaamua kulinganisha na maisha kabla hajaondoka ingawa sio kila wakati unahitaji kulinganisha ili kujua ukweli.

Hayo mawili yanaweza yasikupe sura halisi ya Luis! Mimi namtazama Luis kama mchezaji mpya kwenye ligi yetu yaani kama alivyo Onana, Max na wengine.

Ligi imebadilika wapo wachezaji alikuwa nao timu moja [Simba] maana yake walikuwa daraja moja na kama walipishana basi ni kidogo hapa utawataja wachezaji kama [Kagere,Onyango,Mugalu, Ndemla,Gadiel nk] leo hii hao wachezaji hawapo tena Simba, wameondoka wamekuja wapya wa daraja lingine ambao Klabu wanaona wanaendana na malengo yao kwa sasa .

Wale walioondoka wameenda sehemu nyingine wamekuwa chaguo la kwanza maana yake hata kwenye upinzani anakutana na wapinzani wa daraja la juu, Yanga hii ya 2023 sio ile waliyoifunga nne Nusu fainali ASFC same to Azam na timu zingine zilizopo kwenye ligi.

Mimi binafsi nitatoa hukumu ya kiwango cha Luis, mwisho wa msimu kwa sasa acha acheze mpira.

Namba: Hadi sasa assist 3 , mechi 6 assist mbili kati ya hizo zimeamua mchezo na ndio mchezaji kinara wa kutoa assist kwenye kikosi cha Simba

Chanzo: www.tanzaniaweb.live