Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miquissone: Ubingwa wa VPL nyie chongeni

Luis Pic Data Miquissone: Ubingwa wa VPL nyie chongeni

Thu, 11 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

By Thobias SebastianMore by this Author KATIKA toleo lililopita Luis Miquissone alielezea dili lake na klabu za Uarabuni, lakini akahitimisha kwamba Simba ndiyo yenye uamuzi wa kumuuza au kutomuuza kwavile ana mkataba mrefu nao.

Katika muendelezo wa leo Luis anaanza na ishu yake na Yanga;

Simba baada ya kucheza mechi ya kwanza na UD Songo ugenini Msumbiji, kilifanya kikao na Luis ambaye alieleza kuhusu masuala yake yote ya kimkataba ili kupatikana.

Baada ya hapo Simba hawakuendelea kwa spidi ya kumtaka. Kumbe Yanga pia walikuwa wakimhitaji na wakaingia kikamilifu ili kumnasa winga huyo ambaye alionyesha kiwango bora zaidi katika mechi ya marudiano na Wekundu wa Msimbazi iliyopigwa Dar es Salaam.

Simba wakastukia mchongo kwamba Luis anatakiwa na Yanga, ambao walifikia hatua ya kujiamini kwamba watainasa saini yake. Jambo hilo liliwastua Simba. Mara hii Wekundu wa Msimbazi wakarudi kwake kwa nguvu kubwa zaidi.

Yanga walipotuma wawakilishi wao Msumbiji alikokuwa anaishi Luis, wakaambulia patupu kwa sababu Simba walishamtorosha.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz