Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miquissone, Niyonzima kuliamsha leo

Niyonzima+pic Miquissone, Niyonzima kuliamsha leo

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

LEO saa 10 kamili kwenye uwanja wa mkoa wa Nyamirambo nchini Rwanda kutakua na mechi ya kukata na shoka itakayo wakutanisha mastaa kutoka Ligi Kuu Tanzania bara Luis Miquissone dhidi ya Haruna Niyonzima  na Meddie Kagere.

Ni mechi ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (Afcon) kati ya Timu ya Taifa ya Rwanda 'Amavubi' yenye Nyota wa Simba Kagere na Niyonzima wa Yanga dhidi ya Msumbiji yenye nyota wa Simba Miquissone.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani pia wenye uungwana kutokana na ukaribu wa wachezaji hao watatu hususani wakiwa katika klabu zao nchini Tanzania.

Wachezaji wote hao wamewahi kucheza Simba huku Kagere na Niyonzima wakicheza pamoja kwa zaidi ya msimu mmoja katika klabu hiyo mwaka  2017 hadi 2019 pia Kagere na Miquissone wakicheza wote mpaka sasa kwa wekundu hao wa Msimbazi.

Timu zote mbili zipo kwenye kundi F  zikiwa sambamba na timu za Cameroon na Cape Verde na Rwanda katika mechi ya leo watahitaji kupata ushindi ili kufufua matumaini ya kusonga mbele kwani hadi sasa hawajashinda mchezo hata mmoja kati ya minne waliyocheza wakitoa sare mbili na kupoteza mbili tofauti na wapinzani wao Msumbiji ambao angalau wameshinda mechi moja na kupata sare moja katika mechi nne walizocheza.

Hata hivyo Msumbiji wana rekodi nzuri mbele ya Amavubi Stars kweni kwenye mchezo wa kwanza waliocheza nyumbani waliibuka na ushindi wa  2-0 mabao yakifungwa na Stelio Ernesto dakika ya 28 na Mexer sitoe dakika ya 31.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz