Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mipira mitatu, jahazi moja

Aziz Fei Tena Mipira mitatu, jahazi moja

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jana pale Lupaso yale magoli matatu yamenikumbusha ile vita ya riziki kati ya Jahazi na ufunguo, yamenikumbusha maumbile hayawezi kutoa riziki na vipawa sawa kwa watu wawili tofauti ambao hawakupuliziwa pumzi sawa, na hakika riziki imekaa mkao wa ngazi yaani wa juu anapata zaidi na wa chini anapata kidogo.

Inawezekana ufunguo ni bora mbele ya ufunguo na Jahazi ni bora nyuma ya jahazi lakini riziki kamwe haiwezi kuwa na hesabu sawa kuna muda wale wanaopata sana sio kwasababu wana juhudi isipokuwa Mwenyezi Mungu ameamua kuwapa kwa upendo tu na wale wanaopata kwa uchache Mwenyezi Mungu ameamua kuwapa tu fumbo nyeti kuhusu maisha.

Najua riziki ya ufunguo ilihusishwa sana na riziki ya jahazi kwasababu wavivu wa kufikiri waliamua kuingilia kazi ya Mwenyezi Mungu,Wavivu wa kufikiri mbaya zaidi walisahu kwamba kila mtu atalipwa dhambi zake kwa kiwango sawa na rikizi yake.

Jana nimeikumbuka sana leo kwasababu kiwango bora cha Jahazi na uroho wa kufunga wa Ufunguo umerudisha mkanda nyuma kwenye hadithi ya riziki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live