Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mipango ya Yanga kuiua Ihefu kesho, Musonda kuanza

Kaze Mwamnyeto Mwamnyeto na Kaze

Sun, 15 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kesho kati ya Yanga Sc dhidi ya Ihefu FC, kocha msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze na nahodha Bakari Mwamnyeto wamefanya mkutano na waandishi wa habari leo Jumapil, Januari15, 2022.

Cedric Kaze amnaye ni raia wa Burundi ndio alikuwa wa kwanza kuzungumza na kueleza maandalizi pamoja na wachezaji watakaokosekana kwenye mchezo wa kesho.

TOFAUTI YA MCHEZO HUU NA ULE WA RAUNDI YA KWANZA

"Tunajua ni mechi itakayokuwa na ushindani mkubwa, tunaamini tunakwenda na kukutana na timu tofauti na ile iliyocheza mzungukO wa kwanza Tumeona wamesajili wachezaji wengi hivyo tumejiandaa na ushindani mkubwa zaidi.

"Kila pointi ni muhimu kwetu kwenye mechi zilizobaki na hii ndio sababu tunakwenda kupambana tuwe na kiwango kizuri kesho na tupate pointi tatu," amesema Kaze.

NINI KIMEBADILIKA KWA YANGA KWENYE MCHEZO HUU

"Tulipoteza mechi ya kwanza mbele ya Ihefu lakini naamini mazingira ya kesho yatakuwa tofauti na mwanzo.

"Mechi ya kwanza kulikuwa na mazingira magumu hasa kwenye uchovu wa wachezaji kutokana ma mechi nyingi mfululizo.

"Lakini kwa mchezo wa kesho tumepata muda wa kutosha wa kupumzika, tuko tayari kimwili na kiakili kupambana kesho kupata pointi 3."

WACHEZAJI WATAKAOKOSEKANA

"Tutawakosa Yanick Bangala, Stephane Aziz Ki na Benard Morrison lakini golikipa Abuutwaleeb Mshery ambaye alianza mazoezi amepata majeraha tena, hivyo hatakuwa sehemu ya mchezo. Tutamkosa pia Zawadi Mauya ambaye ameumia."

NYOTA WAPYA WANAWEZA KUTUMIKA

"Mpaka sasa tumefanya mazoezi pamoja na Mudathir na anaweza kuwa sehemu ya kikosi cha kesho, Kennedy tunaendelea kuangalia utimamu wake tuone kama ataweza kujumuika na wenzake kesho."

NENO LAKE KWA MASHABIKI

"Tumekuja na nahodha kwenye mkutano wa leo kuonyesha jinsi gani tumeweka uzito kwenye mchezo wa kesho. Tuko tayari kimwili na kiakili kupambana kwa pointi 3 za kesho!,"amesema Kaze.

Kwa upande wa nahodha wa Yanga, Bakari Nondo Mwamnyeto alisema; "Mashabiki waje kwa wingi uwanja wa Mkapa, wachezaji tuko tayari na tunaamini tutapambana kuwapa furaha mashabiki wetu."

Mchezo wa kesho utaanza saa 12:30 jioni kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, na tiketi tayari zimeshaanza kuuzwa kwenye vituo tofauti tofauti jijini Dar Es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live