Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mipango ya Liverpool, Chelsea yavurugwa

Gfcdrxgfdgc Mipango ya Liverpool, Chelsea yavurugwa

Thu, 13 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Licha ya Liverpool na Chelsea kuonyesha nia ya kutaka kumsajili katika dirisha hili, mtendaji mkuu wa Shakhtar Donetsk amesisitiza kwamba timu hiyo haina mpango wa kumuuza kiungo wake, Georgiy Sudakov katika dirisha hili la majira ya kiangazi.

Sudakov ni mmoja kati ya mastaa tegemeo wa kikosi cha kwanza cha Shakhtar na msimu uliopita aliiwezesha kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amempa ruhusa ya kuondoka beki wa timu hiyo Joao Cancelo ambaye amerejea kwenye timu baada ya kuhudumu kwa mkopo kwenye kikosi cha Barcelona katika dirisha lililopita.

Cancelo aliomba kuondoka Man City kwa sababu hakuwa anapata nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha matajiri hao wa Jiji la Manchester, mkataba wake unamalizika mwaka 2027.

WOLVES, Southampton na Everton ni miongoni mwa timu zinazoiwania saini ya straika wa Chelsea na Albania, Armando Broja katika dirisha hili.

Staa huyu ambaye msimu uliomalizika alicheza kwa mkopo wa miezi sita Fulham, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Msimu huu amecheza mechi 27 za michuano yote na kufunga mabao mawili.

KABLA ya kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea RB Leipzig, staa wa timu hiyo Benjamin Sesko alikuwa akihitajika na Arsenal lakini alikataa kujiunga nayo.

Arsenal ilikuwa ikitaka kumsajili Sesko kwa ajili ya kuboresha eneo lao la ushambuliaji ambalo ni kipaumbele chao kwa sasa.

Kumkosa staa huyo kutavuruga mipango ya Gunners.

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Mason Greenwood anadaiwa kukataa ofa ya kujiunga na Fenerbahce katika dirisha hili kwa sababu hahitaji kufundishwa na Jose Mourinho anayetarajiwa kutangazwa kuwa kocha mpya wa timu hiyo katika siku chache zijazo.

Greenwood ambaye msimu uliomalizika alikuwa akicheza kwa mkopo Getafe, mkataba wake na Man United unamalizika mwaka 2025.

NEWCASTLE United inaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kumsajili mshambuliaji wa Brentford na Cameroon, Bryan Mbeumo, 24, katika dirisha hili. Timu hizi zinataka kumsajili Mbeumo baada ya kuvutiwa na kiwango bora alichoonyesha tangu kuanza kwa msimu uliomalizika ambapo alicheza mechi 27 za michuano yote na kufunga mabao tisa.

ARSENAL inataka kutuma wawakilishi wake kwenda Hispania kuzungumza zaidi na Barcelona kwa ajili ya kuipata saini ya beki wa timu hiyo na Senegal Mikayil Faye, 19, katika dirisha hili.

Staa huyu amevutia timu nyingi kutokana na kiwango alichoonyesha msimu uliomalizika ambapo alicheza mechi 33 za michuano yote.

Mkataba wa Mikayil unatarajiwa kumalizika mwaka 2027, Arsenal imeonyesha nia ya kumsajili baada ya kiwango bora alichoonyesha akiwa na timu za vijana za Barca.

Chanzo: Mwanaspoti