Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Minziro awatangazia hali ya hatari Dodoma Jiji

Geita Gold FC FCFC Minziro tambo tupu akiwavaa Dodoma Jiji, Ligi Kuu Bara!

Mon, 13 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Geita Gold Fred Felix 'Minziro' ameipiga mkwara Dodoma Jiji wakati wakikabiliana leo katika mfululizo wa Ligi Kuu Bara, huku wageni wao nao wakijibu mapigo kwamba wasitarajie mteremko kwenye Uwanja wa Nyankumbu, mjini Geita.

Geita inashika nafasi ya tano katika msimamo ikiwa na pointi 36, huku Dodoma ikiwa ya 11 ikiwa na alama 31, timu zote zikiwa zimecheza michezo 26.

Mchezo wa duru la kwanza uliofanyika Uwanja wa Jamhuri timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1 mabao ya Dan Lyanga dakika ya 75 kwa Geita na Waziri Junior dakika ya 90 kwa Dodoma Jiji, lakini leo zikienda kurudiana, Minziro alisema anaiheshimu Dodoma na anaamini utakuwa ni mchezo mgumu lakini amejipanga kuondoka na alama tatu.

"Sina majeruhi hata mmoja, wachezaji wangu wote wapo freshi kesho (leo) tuombe uzima," alisema, wakati kocha msaidizi wa Dodoma, Mohammed Muya alitamba licha ya kuwakosa mawinga Issa Abushehe na Omary Kanyoro na mshambuliaji, Omary Nassoro 'Dagachenko' kutokana na kuwa majeruhi, bado anaamini watashinda.

Kocha huyo alisema, kiungo Cleophace Mkandala mabeki Augustino Nsata na Abubakary Ngalema wana hatihati ya kucheza kwani ndio wameanza mazoezi kutoka majeruhi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live