Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Minziro awalaumu wachezaji wake kichapo cha 3-1 dhidi ya Simba

Minziro  323.png Minziro awalaumu wachezaji wake kichapo cha 3-1 dhidi ya Simba

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Tanzania Prisons, Fred Minziro, amewalaumu wachezaji wake kufuatia kichapo walichotandikwa na Simba SC 3-1.

Kocha huyo ametoa kauli hiyo Oktoba 5, 2023 mara baada ya kumazika kwa mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

"Ni kukosa umakini, ni makosa yale yale yamejirudia ambayo nimekuwa nikiwaelekeza mazoezini, ukiangalia goli la kwanza na hata la pili ni makosa yale yale, wachezaji wakubwa kama hawa wa Simba ukiwapa nafasi kama vile lazima wakuadhibu," alisema Minziro.

Tanzania Prisons wamebaki mkiani mwa Ligi Kuu wakiwa na alama 1 pekee huku Simba wakikwea kileleni na alama zao 12 baada ya kushinda mechi zote nne za msimu huu wa Ligi Kuu ya NBC 2023-24.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live