Beki wa kati, Shown Oduro raia wa Ghana leo kwa mara ya kwanza ataitumikia timu hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu tangu asajiliwe dirisha kubwa huku kiungo Mjapani, Shinobu Sakai akianzia benchi.
Geita Gold itavaana na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu kuanzia saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Nyankumbu, Geita huku mastaa hao wa kigeni wakiwa sehemu ya kikosi kwa mara ya kwanza tangu wasajiliwe kutokana na kukwamishwa na vibali vya kazi.
Katika mchezo huo, Kocha Mkuu wa Geita Gold, Felix Minziro amefumua kikosi kilichocheza na Yanga kwa kufanya mabadiliko ya wachezaji watatu huku Nahodha, Dany Lyanga akikosekana.
Wachezaji waliobadilishwa ni beki wa kati, Oscar Masai, beki wa kushoto, Adeyum Salehe na winga, Raymond Masota ambapo mtanange huo unasubiriwa huku kukiwa na uwezekano wa mvua kubwa kushuka muda wowote.
Baadhi ya nyota waliotajwa kutokuwepo kambini kutokana na madai ya mishahara, Saido Ntibazonkiza, Sebusebu Samson na Oscar Masai wapo na ni sehemu ya wachezaji watakaocheza leo.
Huku kiungo wa kikosi hicho, Kelvin Nashon, beki, Haruna Shamte na kiungo mshambuliaji, Seleman Ibrahim waliokuwa nje wakiuguza majeraha nao wakirejea leo.
Kikosi cha Geita Gold kinachoanza leo ni; kipa Arakaza McArthur, George Wawa, Yahya Mbegu, Shown Oduro, Kelvin Yondani, Kelvin Nashon, Juma Mahadhi, Yusuph Kagoma, Saido Ntibanzokiza, Geoffrey Manyac na Offen Chikola.
Wachezaji wa akiba ni Sebusebu Samson, Adeyum Salehe, Haruna Shamte, Oscar Masai, Raymond Masota, Seleman Ibrahim, Erick Yema, Edmund John na Shinobu Sakai.