Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Minziro akataa uteja kwa Yanga

Fred Felix Minziro Kocha Mkuu wa Geita Gold FC Fred Felix Minziro

Sat, 8 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Geita Gold FC, Fred Felix Minziro amesema wapo tayari kwa mchezo wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ dhidi ya Mabingwa watetezi Yanga SC.

Kocha Minziro amesema tayari ameshawapa mbinu zote wachezaji wake, kwani anajua wanakutana na vigogo, lakini wamejipanga kupambana kiume ili kupata ushindi kwa mara ya kwanza mbele ya Yanga SC aliyokiri ina kikosi imara.

“Huwa nawaambia wachezaji kutorudia makosa ambayo wameyafanya katika michezo iliyopita hii ndio njia pekee wanaweza kushinda kama watarekebisha makosa, matumaini yetu ni kufanya vizuri kwani hatuishi na matokeo ya yaliyopita kwani mchezo huu kwao ni mpya kabisa,” alisema kocha aliyewahi kuwa nyota na kocha wa Young Africans sambamba na kuzinoa timu nyingine kadhaa nchini.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live