Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Minziro: Tukutane Kaitaba Ligi Kuu

Kagera Sugar Players Minziro: Tukutane Kaitaba Ligi Kuu

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Tukutane Ligi Kuu’. Ni kauli ya Kagera Sugar baada ya kuondoshwa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Namungo ikieleza kwa sasa akili na nguvu zinahamia Ligi Kuu.

Timu hiyo ikicheza jana kwenye Uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi iliondoshwa kwenye michuano hiyo kwa penalti 5-4 baada ya dakika 90 kuisha kwa suluhu ya bila kufungana.

Matokeo hayo yaliifanya Namungo kutangulia robo fainali ya kombe hilo ikiungana na Geita Gold walioitoa Rhino Rangers kwa mabao 2-1 na Tabora United iliyoifumua Singida FG jioni ya leo kwa mabao 3-0.

Kagera iliyopo nafasi ya nane kwa pointi 24, inatarajia kurejea uwanjani Aprili 14 kuwakabili Dodoma Jiji kwenye mchezo wa Ligi Kuu utakaopigwa Kaitaba mjini Bukoba.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Fred Felix ‘Minziro’ amesema malengo yao ilikuwa ni kufika fainali ya michuano hiyo, lakini vijana licha ya kupambana, haikuwa bahati yao.

Alisema kuondoshwa katika michuano hiyo inawapa hasira na kuelekeza nguvu na akili zao kwenye Ligi Kuu kuhakikisha wanashinda mechi zilizobaki na kujiweka pazuri.

“Vijana walipambana licha ya kukosa nafasi nyingi walizopata, lakini haikuwa bahati yetu, tunaenda kujipanga na kusahihisha makosa ili mechi za Ligi Kuu tufanye kweli,” amesema Minziro.

Kocha huyo aliongeza kabla ya mechi dhidi ya Dodoma Jiji wataisuka vyema safu ya ushambuliaji kuhakikisha wanapopata nafasi ya bao hawaachi kitu ili kufikia malengo.

Chanzo: Mwanaspoti