Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Minziro: Hatuiogopi Yanga Tutawafunga Wakiwa Wamesimama

Fred Felix Minziro Minziro

Wed, 23 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KOCHA Mkuu wa Geita Gold, Fred Minziro amesema haihofii Yanga watakapokutana kwenye mechi ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam.

Minziro ambaye licha ya kuisifia Yanga kwa usajili wao mzuri msimu huu, ameeleza pia wao hawataiogopa timu hiyo na watashindana nayo ili wapite kucheza nusu fainali.

“Kwanza tunamshukuru Mungu kwa kuingia hatua ya robo fainali maana haikuwa kazi rahisi na ni nafasi nzuri kwetu kuendelea kuitangaza Geita. Lakini kikubwa ni kwamba timu yoyote ikifanya usajili mzuri unawapa alama zao.

“Yanga wamefanya usajili mzuri na hakuna asiyefahamu kwamba wana timu nzuri, lakini yote kwa yote hatuwezi kuwaogopa kwa sababu wao wana timu nzuri, kikubwa na sisi tutatoa ushindani kuhakikisha tunatinga nusu fainali,” amesema Minziro.

Mbali na timu hizo, mechi nyingine za robo fainali za michuano hiyo zitakuwa ni Simba dhidi ya Pamba. Azam itaivaa Polisi Tanzania na Coastal Union itapepetana na Kagera Sugar. Mechi hizo zinatarajia kuchezwa kati ya Aprili 8 mpaka 13, mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live