Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mino Raiola afanya kikao cha Siri na Barcelona kuhusu Haaland

Raiola Mino Raiola afanya kikao cha Siri na Barcelona kuhusu Haaland

Sat, 26 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Barcelona imefanya kikao cha siri na wakala Mino Raiola ambapo walizungumzia juu ya uhamisho wa wachezaji akiwemo mchezaji wa klabu ya Borussia Dortmund Erling Haaland.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa norway amehusishwa na vilabu vingi vikubwa barani Ulaya vikiwemo Barcelona, Man City na Real Madrid huku kwenye mkataba wake kukiwa na kipengere cha kuuzwa kwa £64 million.

Kulingana na taarifa zilizotolewa na De Telegraaf, raisi wa klabu ya Barc Joan Laporta na mkurugenzi wa ufundi Jordi Cruff walikuwa na mzungumzo ya siri na Mino Raiola kwenye ofisi yake jijini Monaco.

Haaland mpaka sasa amefanikiwa kufunga goli 16 kwenye michezo 14 ya Bundesliga hadi sasa kwenye msimu huu, pia kwenye mazungumzo hayo klabu ya Barc waligusia uwezekano wa kumpata beki wa klabu ya Ajax Noussair Mazraoui.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live