Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Minamino aipeleka Liver Robo Fainali FA

Liverpool Versus Norwich 1 Wachezaji wa Liver wakimpongeza mfungaji wa Magoli Takumi Minamino

Thu, 3 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa Kombe la Carabao, Timu ya Liverpool wamefanikiwa kutinga Robo Fainali ya Kombe la FA England baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Norwich City usiku wa Jumatano Uwanja wa Anfield.

Mabao ya Liverpool yote yamefungwa na Takumi Minamino dakika ya 27 na 39, wakati la Norwich City limefungwa na Lukus Rupp dakika ya 76.

Huenda ikawa ni safari nyingine kwa vijana wa Jurgen Klopp kujikusanyia mataji England baada ya wiki iliyopita kubeba Kombe la Carabao Cup.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live