Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Milovan Katimuliwa Ghana

Milovan Rajevac Milovan Katimuliwa Ghana

Sat, 22 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

BAADA ya kupata matokeo mabaya ya Ghana katika michuano ya AFCON inayoendelea, Wizara ya Michezo ya nchi hiyo katika mkutano wa dharura siku ya Ijumaa iliagiza Chama cha Soka cha Ghana kumfukuza kazi kocha wake Mserbia, Milovan Rajevac.

Licha ya kusitasita kwa FA kumtimua Rajevac, wizara hiyo inaonekana kushinda mzozo kuhusu mustakabali wa Mserbia huyo.

Katika kipindi chake cha kwanza akiwa na Black Stars Rajevac aliiongoza Ghana kutinga fainali za AFCON 2010 na Robo fainali ya Kombe la Dunia la 2010.

Kipindi chake cha pili hakikwenda kama ilivyotarajiwa kwani Ghana walitoka AFCON 2021 bila ushindi, wa kwanza wa aina yake katika historia ya Black Stars.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live