Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Milioni 10 zawapagawisha wachezaji wa Yanga

78865 Pic+mill

Mon, 7 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Nahodha msaidizi wa Yanga, Juma Abdul amesema motisha ya Sh10 Milioni waliyoahidiwa kupewa katika kila ushindi watakaoupata imeongeza morali kwa wachezaji.

Kiungo Abdulziz Makame alifunga bao pekee kwa Yanga ikichapa Coastal Union 1-0 jana kwenye Uwanja wa Uhuru, huo ni ushindi wa kwanza kwa Yanga msimu huu baada ya kucheza mechi tatu wakifungwa moja, sare moja na kushinda moja.

Beki Abdul alisema kitendo kilichofanywa na uongozi kwa kuwapa motisha kutokana na ushindi ni cha kupongezwa na kuwakumbusha wachezaji matokeo mazuri yanahitajika katika kila mchezo.

"Tumepokea kwa furaha na tunaushukuru uongozi kwa njia waliyoamua kuitumia ili kuturudisha katika ushindani na ikiwezekana tuweze kupata nafasi nzuiri ya kuiwakilisha tena nchi katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa mwakani," alisema.

Abdul aongeza kuwa bado wanaendelea kuboresha kikosi huku akibainisha kuwa shida kubwa inayowafanya wakose matokeo ni kukosa muunganiko wa wachezaji ambao anabainisha kuwa kwa asilimia kubwa ni wageni.

 

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz