Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mil 600 zatolewa kurusha NBC Championship

Mil 600 Zatolewa Kurusha NBC Championship Mil 600 zatolewa kurusha NBC Championship

Wed, 13 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia amevitaka vilabu shiriki vya Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) kutumia fursa ya Ligi hiyo kuoneshwa mubashara kwa kujitangaza ili kushawishi wadhamini.

Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya uingiaji mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya Sh Milioni 613, kati ya TFF na kituo cha TV3 kwaajili kuonesha mubashara NBC Championship.

"Ligi ya NBC Championship itakapokuwa inarushwa na TV3 na TV3 Sports, dunia itashuhudia ligi ngumu katika ukanda wa Afrika," amesema Karia.

Rais huyo amesema, hatua zinazopigwa katika mpira wa miguu ni kutokana na mazingira mazuri yaliyowekwa na serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kushawishi wawekezaji zaidi.

Aidha, Msimamizi wa vipindi wa TV3, Emmanuel Sikawa amesema wanaenda kuonesha zaidi ya michezo 170 ya NBC Championship kupitia TV3 na TV3 Sports watakayoizindua siku za usoni.

"Tunatambua waliopita walifanya vizuri lakini sisi tutaenda kuendelea pale walipoishia na kwenye mapungufu tutasahihisha ili kuwa bora zaidi," amesema Sikawa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live