Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mikel Arteta kuingia sokoni Januari 2024

Image 213 1140x640.png Mikel Arteta kuingia sokoni Januari 2024

Sat, 14 Oct 2023 Chanzo: Dar24

Licha ya ubora mkubwa unaoonekana ndani ya kikosi chake, lakini inaelezwa kuwa kocha mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta yuko kwenye mpango wa kuingia tena sokoni Januari 2024, kwa ajili ya kuboresha kikosi chao.

Mikel Arteta ambaye anasifika kwa kuhimiza wachezaji kwa bidii sana katika programu zake za mazoezi mara baada ya kupata ushindi muhimu wa bao 1-0 dhidi ya Manchester City aliwapa mastaa wa timu hiyo mapumziko mafupi.

Arsenal inajipanga tena kuingia vitani kwa ajili ya kusaka saini ya staa wa Brentford, Ivan Toney ambapo inaelezwa kuwa atawagharimu kiasi cha kuanzia Pauni Milioni 60.

Jorginho anatazamiwa kuondoka Arsenal, ili kuongeza wa klabu hiyo kuwa na uwezekano wa kifedha wa kuingia sokoni, huku pia wakitajwa kuwania saini ya winga wa Wolves, Pedro Neto.

Chanzo: Dar24