Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mikel Arteta amsikilizia Alvarez

Arteta X Alvarez Mikel Arteta amsikilizia Alvarez

Sat, 3 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mabosi wa Arsenal wanafuatilia kwa karibu kinachoendelea kati ya straika wa Manchester City, Julian Alvarez na kocha Pep Guardiola ambao hivi karibuni wameingia katika vita ya maneno.

Awali, hakukuwa na taarifa yoyote juu ya Arsenal kutaka kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina, lakini kile kinachoendelea kati yake na Guardiola kimesababisha washika mitutu hao waanze kumtolea macho kwa ajili ya kumsajili.

Hivi karibuni, Alvarez alisema hafurahishwi na kitendo cha kutopata nafasi ya kucheza katika mechi muhimu, hivyo atafikiria juu ya hatima yake mara baada ya kutoka katika michezo ya Olimpiki inayoendelea Ufaransa.

Guardiola alipoulizwa juu ya hilo, alisema hana shida na wala hatamzuia mchezaji yeyote anayetaka kuondoka na kwamba Alvarez afikirie na atakapopata jibu ampigie simu mkurugenzi wa ufundi.

Arteta tayari ameshaanza kujisogeza karibu na staa huyo ambaye kama akimsajili atakuwa mchezaji wa tatu kumchukua kutoka Man City tangu atue Arsenal baada ya Gabriel Jesus na Oleksandr Zinchenko.

Hata hivyo, ili kukamilisha dili hilo Arsenal itatakiwa kutoa zaidi ya Pauni 80 milioni kama ada ya uhamisho,

Kiasi hicho inaweza kutoa ikiwa tu itafanikiwa kuuza wachezaji wawili baada ya Emile Smith Rowe aliyetua Fulham.

Katika dirisha hili la usajili tayari Arsenal imeshafanya usajili wa Pauni 70 kwa kumshusha beki wa Bologna na Italia, Riccardo Calafiori na kumsainisha mkataba wa kudumu David Raya kutoka Brentford, hivyo hawahitaji kutoa pesa nyingi ili kufanya usajili mwingine.

Chanzo: Mwanaspoti