Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mikel Arteta: Albert Stuivenberg Kuingoza Arsenal

Mikel Arteta And Albert Stuivenberg Mikel Arteta (kushoto), na msaidizi wake Albert Stuivenberg

Sat, 1 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mikel Arteta atamuachia majukumu msaidizi wake Albert Stuivenberg kusimamia mchezo dhidi ya Manchester City wakati akiwa anapata matibabu ya ugonjwa wa Uviko-19

Mkufunzi huyo wa timu ya Arsenal alipatikana kwa mara ya kwanza na maambukizi ya Uviko-19 katika kipidi cha March 2020 wakati kukiwa na mapumziko kutokana na katazo la kutokutoka nje kabla ya kupata tena hivi juzi.

Ingawa Mikel Arteta hakuweza kushiriki kwenye mkutano na waandishi wa habari, alikuwa na kusudi la kumruhusu Stuivenberg kuweza kusimamia kila kitu katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya City.

“Ni mtu ambaye yuko karibu na mimi na anaweza, ameshafanya hivyo awali ninaweza kukaa nikiwa na amani, tumeshazungumza bila shaka tutakuwa na mawasilaano, nitamwachia majukumu na kumpa uhuru wa maamuzi akiwa uwanjani.” Alisema Mikel Arteta

Arsenal wameweza kuchukua pointi moja tu kwenye michezo 11 waliyokutana na Manchester City kwenye ligi kuu ya Uingereza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live