Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mikeka yamponza Kocha wa Morecambe FC

John McMahon John McMahon

Fri, 9 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha msaidizi wa klabu ya Morecambe inayoshiriki Ligi daraja la nne Nchini England, John McMahon ameshtakiwa na Chama cha soka Nchini England (FA) kwa utovu wa nidhamu kuhusiana na kamari.

Taarifa ya FA inasema inadaiwa kuwa alikiuka Kanuni ya FA kwa kucheza kamari kwenye mechi za soka mara 251 kati ya tarehe 30 Novemba 2019 na 14 Oktoba 2023.

Katika taarifa fupi msemaji wa klabu hiyo alisema: ‘’Klabu ya Soka ya Morecambe inakubali taarifa ya FA kuhusu mashtaka yaliyotolewa dhidi ya John McMahon. Kwa kuwa hili ni suala linaloendelea, hatutatoa maoni zaidi kwa wakati huu.’’

Chanzo: www.tanzaniaweb.live