Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mikataba ya wachezaji iheshimiwe kuepuka kesi

Bernard Morrison Signs For Simba Sc Pea5nkp57riv1gjc4siy89exb Mikataba ya wachezaji iheshimiwe kuepuka kesi

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesi nyingi ambazo zinawasumbua mabosi wengi wa timu ndani ya ardhi ya Tanzania ni kuhusu malipo. Mikataba ya wachezaji inakwenda kirafiki na hakuna ambaye anajali.

Hili ni janga kubwa ambapo kila siku kumekuwa na kesi zinazowahusu wachezaji kufungua kesi kuhusu malipo yao. Haina maana kwamba waajiri hawatambui umuhimu wa kuwalipa hapana wanaamua kufanya makusudi.

Mwisho wanaamua kuvunja mikataba na wachezaji bila ufuata utaratibu. Kesi zinakuwa nyingi kwa wachezaji kuamua kufungua kesi kuhusu malipo yao.

Ikiwa itakuwa ni tabia kwa timu zote Bongo hili ni tatizo ambalo linahitaji kufanyiwa kazi kwa umakini. Hii itapunguza gharama ambazo zinazikumba timu husika kuwa kwenye sakata ya kulipa fedha baada ya wachezaji kushinda kesi zao.

Muhimu kuzingatia makubaliano ya kwenye mikataba kwa viongozi kuwalipa wachezaji kwa wakati. Stahiki zao ni muhimu kufanyiwa kazi na wanapambana kutimiza majukumu yao wanapopata nafasi.

Muda ni sasa kuendelea kutimiza majukumu ya kazi na kila mmoja atomize majukumu yake kwa wakati. Wachezaji wanakazi kubwa kwa sasa kuendelea kupambana kutimiza majukumu na viongozi wanapaswa kutimiza majukumu yao.

Malipo kwa wakati na kuzingatia taratibu wakati wa kuvunja mikataba hilo litapunguza kesi ambazo zinapatikana mara kwa mara kwenye sekta ya michezo.

Ikiwa wachezaji watalipwa kwa wakati basi itapunguza kesi nyingi kuripotiwa na wachezaji kufungua kesi kila wanapositishiwa mikataba yao na timu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: