Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miili ya 25 waliokufa ajali ya Ngaramtoni kuagwa siku ya maandamano ya Chadema

Ajali M4 WA0026 Miili ya 25 waliokufa ajali ya Ngaramtoni kuagwa siku ya maandamano ya Chadema

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miili ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori la mizigo na magari matatu, iliyotokea katika Barabara Kuu ya Arusha-Namanga Ngaramtoni Kibaoni, jijini Arusha, itaagwa kesho tarehe 27 Februari 2024, kwenye Uwanja Wa Sheikh Amri Abeid.

Ratiba hiyo imetolewa leo tarehe 26 Februari 2024 na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella, akizungumzia hatua zinazoendelea kuhusu ajali hiyo iliyotokea Jumamosi iliyopita.

“Kesho kuanzia saa tatu asubuhi kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, kutakuwa na zoezi la kutoa heshima za mwisho kwa ndugu zetu ambao wanaenda kwenye kupumzishwa. Niwaombe wana Arusha tushirikiane katika zoezi hili la kutoa heshima za mwisho,” amesema Mongella.

Aidha, Mongella amesema shughuli ya kuaga miili hiyo haitaathiri maandamano ya amani yaliyopangwa kufanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

“Niwaombe tuvumiliane kwa kesho, rai yangu kuwaomba viongozi wenzetu wahakikishe hilo maandamano hayo ya hiari. Tunatambua uwepo wa maandamano ya Chadema yapo kisheria na yatasimamiwa kama maeneo mengine,” amesema Mongella.

Ajali hiyo iliyojeruhi watu zaidi ya 20, ilitokea Jumamosi jioni baada ya gari la kubeba mizigo lililokuwa linatokea Namanga kwenda Arusha, kugonga magari matatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live