Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miezi mitatu ya Ronaldo na majanga ya Al Nassr

Cristiano R 7 Miezi mitatu ya Ronaldo na majanga ya Al Nassr

Sun, 30 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Ilikuwa ni katika dirisha lililopita la majira ya baridi, vyombo mbali mbali vya habari Duniani viliandika kuhusu usajili wa Cristiano Ronaldo kwenda Al Nassr ikiwa ni siku kadhaa tangu alipoachana na Manchester United kwa makubaliano ya pande mbili ya kuvunja mkataba.

Mashabiki wengi wa Al Nassr walifurahishwa na usajili wake kwa sababu waliamini angeenda kuwafanya washinde mataji zaidi na kuongeza ubora kwenye timu yao.

Mbali ya kupata umarufu kwenye ikijulikana dunia nzima na kuongeza wafuasi kwenye mitandao yao ya kijamii ikiwa pamoja na Instagram ambapo kabla ya Ronaldo ilikuwa na wafuasi wasiozidi milioni moja lakini sasa ina wafuasi milioni 14.

Vilevile licha ya uwezo kuendelea kuonyesha makali akifunga mabao 14 kwenye mechi 14, bado Al Nassr haijawa na maisha mazuri kwa msimu na sasa ipo kwenye hatari ya kumaliza msimu ikiwa haina kikombe hata kimoja.

Hapa tumekuchambulia majanga na matukio ya kuhuzunisha ambayo yameitokea timu hii tangu imsajili Ronaldo January mwaka huu mbali ya faida ilizopata.

KING CUP

Kwenye michuano ya King Cup, Al Nassr imeishia kwenye hatua ya nusu fainali huku Ronaldo akishindwa kutoa hata pasi ya bao kwenye jumla ya michezo miwili aliyocheza kwenye michuano hiyo.

Safari yao iliishia kwa Al-Wehda kwenye mchezo wa nusu fainali uliopigwa April 24, mwaka huu ambapo walikubali kichapo cha bao 1-0.

Licha ya Al-Wehda kucheza pungufu kwa zaidi ya dakika 30 baada ya beki wao Abdullah Al-Hafith kupewa kadi nyekundu bado Al Nassr ilishindwa kufurukuta na kujikuta imeangukia pua na kuondoshwa.

Hata hivyo msimu huu kidogo umekuwa wa mafanikio kwa Al Nassr kwenye michuano hii kwani mwaka jana iliishia hatua ya robo.

SUPER CUP

Kama ilivyokuwa msimu uliopita, Al Nassr pia imeishia hatua ya nusu fainali kwenye michuano hii kwa msimu huu ambayo ndio hatua ya kwanza.

Saud Super Cup ni michuano inayohusisha timu nne za juu za msimu uliotangulia ambazo zitacheza nusu fainali kisha mbili zitakazopita zitacheza fainali.

Ronaldo ambaye alikuwepo kwenye mchezo huo wa nusu fainali hakufunga hata bao moja kwenye kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Al-Ittihad.

Bao pekee la Al Nassr lilifungwa na kiungo mshambuliaji kutoka Brazil Talisca dakika ya 67.

KIMATAIFA HATARINI

Kawaida ni timu moja tu kutoka Ligi Kuu ya Saud Arabia ndio hupata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabinga nayo ni ile itayomaliza nafasi ya kwanza na kuchukua ubingwa wa nchi hiyo.

Kwa sasa Al Nassr inashika nafasi yapili ikiwa na alama 53 baada ya kucheza mechi 24 dhidi ya Al Ittihad inayoongoza kwa pointi 56 ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Mbaya zaidi ni kwamba kwenye mechi saba zilizosalia kabla ya msimu kumalizika itakuwa na mechi tatu ngumu za dhidi ya Al Fateh, Al shabab na Al Ta'ee. Kutokana na kiwango chao cha sasa inaonekana kuwa huenda wakaangusha alama.

KIMENUKA RONALDO NA BENCHI LA UFUNDI

Kutokana na kiwango kibovu cha timu hiyo, mabosi wa Al Nassr walifikia uamuzi wa kumuondosha kocha wao Mfaransa Rudi Garcia ikiwa ni miezi 10 tangu imuajiri.

Baada ya kuondoka kwa Rudi sasa timu hiyo ipo chini ya Dinko Jelicic ambaye kabla ya hapo alikuwa wa timu ya vijana umri chini ya miaka 19 ya matajiri hao.

Uhusiano baina yake na kocha huyu wa muda sambamba na benchi la ufundi la Al Nassr hauonekani kuwa mzuri sana kutokana na aina ya matukio ambayo yanaendelea.

Mfano, wakati wa mapumziko katika mchezo wa nusu fainali ya King Cup Ronaldo alionekana akimfokea kocha wake ikiwa ni ishara ya kutoridhishwa na kiwango cha timu katika kipindi cha kwanza.

Chanzo: Mwanaspoti