Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miezi 5 ya Kaze Yanga, sababu za kutimuliwa zafichuka

Kaze Picha Shabki Data Miezi 5 ya Kaze Yanga, sababu za kutimuliwa zafichuka

Wed, 10 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

By Waandishi WetuMore by this Author Dar es Salaam. Maisha ya ukocha ndani ya Yanga kwa Cedrik Kaze yamefikia mwisho juzi, baada ya miamba hiyo kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Polisi Tanzania.

Matokeo hayo yalikuwa miongoni mwa mwenendo mbivu wa kikosi hicho kwenye mzunguko wa pili, ambao alifanikiwa kushinda mchezo mmoja kati ya sita aliyoshuka uwanjani, akiwa na sare tano na kipigo mara moja.

Yanga, ambayo ilikuwa na matumaini ya ubingwa msimu huu baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza ikiwa juu kwa tofauti mbili, endapo Simba ingeshinda viporo vyake.

Lakini ilijikuta katika wakati mgumu baada ya kulazimishwa sare dhidi ya Mbeya City (1-1) Tanzania Prisons (1-1), Kagera Sugar (3-3), kisha kushinda dhidi ya Mtibwa (1-0), ikafungwa na Coastal Union (2-1) na juzi kulazimishwa sare ya 1-1 na Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Mchezo huo, ulikuwa wa lazima kwa kaze kuibuka na ushindi ili kutuliza presha ya mashabiki na uongozi katika kurudisha pia imani ya ubingwa msimu huu.

Lakini licha ya kuongoza kipindi cha kwanza kwa bao safi la mshambuliaji wa Burundi, Fiston Abdulrazak, ilijikuta ikiruhusu bao hilo kurudi dakika moja kabla ya mchezo kumalizika, lililofungwa na nyota wao wa zamani, Pius Buswita.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz