Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Michuano ya Ngao ya Jamii 2023/24 kupigwa Mkwakwani Tanga

Wallace Karia Rais wa TFF, Wallace Karia

Mon, 3 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea shindano la Ngao ya Jamii 2023-24 ambalo litashirikisha timu 4, Rais wa TFF, Wallace Karia amesema shindano hilo linaloashiria kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC pamoja na mashindano mengine, litapigwa katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

“Kwenye Ngao ya Jamii ambayo msimu huu zitachezwa mechi tatu, mbili za Nusu Fainali na moja ya Fainali, mechi zote zitachezwa Mkwakwani Tanga kwa sababu uwanja wa Uhuru na Benjamin Mkapa vimefungwa na uwanja wa Mkwakwani upo karibu na katika utaratibu mzuri.” - Wallace Karia

Ikiumbukwe mnamo Agosti 2022 bodi ya Ligi TPLB ilibadili utaratibu wa shindano la Ngao ya Jamii kutoka mfumo wa timu mbili na kuwa timu nne.

Timu tatu za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu na Bingwa wa Kombe la Shirikisho zitaunda timu hizo nne. Taarifa ya TPLB ilieleza ikiwa Bingwa wa kombe la Shirikisho atakuwa miongoni mwa Washindi wa nafasi tatu za juu basi timu iliyoshika nafasi ya nne itashiriki shindano hilo.

TIMU ZITAKAZOSHIRIKI NGAO YA JAMII 2023-24

-Yanga SC (Mabingwa)

-Simba SC (Nafasi ya Pili )

-Azam FC( Nafasi ya Tatu)

-Singida Fountain Gate(Nafasi ya Nne)

HATUA YA NUSU

Simba vs Azam

Yanga vs Singida

FAINALI

Mshindi wa mchezo wa Simba/Azam dhidi ya mshindi wa Yanga/Singida.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live