Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Michuano ya Mapinduzi yaingiza mil 496/=

7b82bee995c984463d03d3b28292cfc4 Michuano ya Mapinduzi yaingiza mil 496/=

Mon, 25 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

JUMLA ya Sh milioni 496 zimekusanywa katika michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyomalizika hivi kaibuni mjini Zanzibar.

Michuano hiyo ambayo iliyoshirikisha timu tisa, ilimalizika Januari 13 mwaka huu huku vigogo Yanga wakitwaa ubingwa huo baada ya kuwafunga Simba kwa penalti 4-2.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa VIP kwenye Uwanja wa Amaan Katibu wa kamati ya mashindano hayo, Imane Duwe alisema kuwa fedha hizo zinatokana na makusanyo ya milangoni pamoja na wadhamini.

Alisema kuwa kati ya fedha hizo, makusanyo ya milangoni ni Sh milioni 256 wakati wadhamini walitoa Sh milioni 239, huku Azam pekee wakitoa Sh milioni 150.

Alifahamisha kwamba katika fedha za milangoni, Sh milioni 79.2 ni makusanyo yaliyotokana na mchezo wa fainali kati ya Simba na Yanga.

Aidha, alisema kuwa katika fedha hizo walitumia Sh milioni 354 kwa shughuli mbalimbali, ikiwemo gharama za taa ambazo kwa siku wanatumia Sh milioni 1.5

Matumizi mengine ni pamoja na gharama za kuwalipa waamuzi, malazi, chakula kwa timu pamoja na usafiri wa ndani, ambao kwa siku walikuwa wakilipa Sh 150,000.

Hata hivyo, alisema kuwa mbali na matumizi hayo fedha ambazo zimebakia ni Sh milioni 141.7.

Akizungumzia kuhusu mashindano yote kwa jumla alisema yalifanikiwa kwa kiasi licha ya changamoto ndogo ndogo ambazo zilijitokeza.

Timu zilizoshiriki michuano hiyo ni Simba, Yanga, Azam, Namungo na Mtibwa kutoka Tanzania Bara wakati Zanzibar zilikuwa Mlandege, Malindi, Jamhuri na Chipukizi.

Chanzo: habarileo.co.tz