Kocha wa Uganda, Milutin Sledjovic Micho ametoa shutuma kwa Algeria na Tanzania kuwa ni kama walipanga kutoka sare kwenye mchezo wao uliopigwa dimba la Annaba uliofanikisha Tanzania kufuzu AFCON.
Micho anadai kuwa ni kama Algeria walipanga na Tanzania kufanya hivyo ili kuirahisishia Taifa Stars kufuzu na wao kuangukia pua licha ya timu yake kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Niger.
Kocha huyo raia wa Serbia ameomba Algeria na Tanzania kutolea ufafanuzi suala hili na abainike aliyehusika na suala zima na haamini kama Tanzania walipata sare kwa uwezo wao.
Aidha aliongeza kuwa kila mmoja anatambua DNA ya kocha wa Algeria, Djamel Belmadi katika suala zima la kusaka ushindi hivyo aamini kama Tanzania walipata sare kwa uwezo.
Alhamisi iliyopita, Taifa Stars ilifanikiwa kufuzu fainali za AFCON 2023 baada ya kutoa sare ya bila kufungana na ALgeria ambao tayari walikuwa wameshafuzu huku Uganda na Niger wakitolewa nje ya michuano hiyo licha ya Uganda kushinda kwa bao 2-0.