Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MichezoPatrice Motsepe kuichukulia hatua kali Mamelodi Sundowns

Dahane Beida Mauritanian referee Dahane Beida

Tue, 9 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni kweli kwamba baadhi ya wachambuzi wameibuka na kudos kuwa mfumo wa Uefa Msaidizi wa Video (VAR) ulronyesha mpira uliopigwa na Stephane Aziz Ki katika dakika ya 59 haukuvuka mstari wa lango na hivyo Yanga hawakustahili bao hilo katika mchezo wao wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns uliofanyika Ijumaa jijini Pretoria.

Mwishoni timu hizo zilimshindwa tena kufungana na mchezo huo kuamuliwa kwa matuta ambazo wenyeji walishinda kwa penati 3-2 hivyo Yanga kuyaaga mashindano hayo kwa uchungu.

Kwa kawaida waendeshaji wa mfumo huo hutakiwa kuwapa watangazaji wa mchezo picha za marudiano zinazoonyesha tukio kutoka pande zote na pale panapostahili picha zigandishwe au kutembea taratibu hufanya hivyo ili si tu mwamuzi zone kwa usahihi zaidi, bali hata watazamaji wa mechi wadhihirishiwe na hivyo uamuzi kuwa wa uwazi.

Lakini hakuna picha za marudio za mfumo huo zilizoonyeshwa kwenye runinga katika tukio hilo zaidi ya zile za marudio za shirika lililopewa haki ya kurusha moja kwa moja matangazo ya mchezo huo na embalo linaweza kuwaitíes na Kamera za kutosha.

Kibaya zaidi, refa msaidizi aliyekuwa anasimamia mfumo huo, hakumtaka mwamuzi wa kati aende kwenye Runinga iliyokuwa uwanjani kujiridhisha kuwa mpira huo haukuvuka kama walivyowasiliana naye.

Mfumo wa VAR ni tofauti na teknoloji ya mstari wa goli (Goal line Teknology) amber haumpi mwamuzi nafasi ya kujiridhisha iwapo kuna utata kuhusu mpira kuvuka mstari wa goli na badala yake refa hutumiwa ishara ndani ya sekunde kumi kuhusu utata wa mpira kuvuka mstari wa goli.

Mwamuzi wa mchezo wa Ijumaa hakutumiwa taarifa na teknolojia hiyo na pengine haikuwa imefungwa kwenye uwanja huo wa Loftus Verseld badala yake alisimamisha mchezo huo wakati kipa alipouwahi mpira uliokuwa unaelekea nje ya uwanja badala ya kuokolewa na beki wake katika tukio hilo.

Hiyo ilikuwa fedheha kubwa inayosababisha kila mara timu kutoka Afrika Kaskazini Kuomba mechi zao zichezeshwe na waamuzi kutoka nje ya bara la Afrika.

Lawama na fedheha kama hizi hazistahili kuendelea katika soka la Afrika ambalo limeanza kupata wawekezaji wa uhakika wanaoweza kuupeleka mpira wetu huu mbali zaidi ikiwa utatatuliwa na uwazi na haki.

Kwa maana hiyo CAF wanatakiwa kukomesha uozo huu na kulisafisha soka la Afrika ili livutie wawekezaji zaidi na kuwapa imani zaidi mashabiki ambao katika baadhi ya viwanja wamekuwa adimu, pengine kutokana na kutoridhishwa na uendeshaji wa mchezo huu maarufu duniani.

Ni muhimu sana kwa Rais wa CAF Patrice Motsepe na timu yake kuchukulia suala hili kwa umuhimu zaidi kuliko hata hayo mambo ya kuanzisha mashindano mengine wakati bado bara linasuasua katika mambo muhimu ya uamuzi.

Tukio hili linamuhusu zaidi Motsepe kama Rais na kama mmiliki wa Mamelodi Sundowns ambaye amekuwa akifanya jitihada kubwa kutetea mpira wa miguu Afrika (AFL;) na hata kupigia debe kupanuliwa kwa mashindano ya klabu Bingwa ya Dunia.

Lakini pia kuhusu Motsepe kama mmiliki wa Mamelodi Sundowns ambayo imenufaika na ubovu wa makusudi ama kizembe wa mwamuzi waliochezesha mchezo huo.

Ili kujisafisha Motsepe hana buda kuhakikisha uchunguzi wa kina unafanyika na ukweli kuweka bayana badala ya jumba boyu kumuangukia au kuwaangukia waamuzi pekee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live