Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Michezo 9 tu yamtenganisha Alonso na Ubingwa wa Bundasliga

Xabi Alonso .jpeg Kocha wa Bayern Liverkusen, Xabi Alonso

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Bayern Munich kupokea kichapo cha goli 3-2 dhidi ya Bochum sasa rasmi wameachwa alama nane (8) na kinara wa msimamo wa Ligi kuu nchini Ujerumani Bayer Leverkusen.

Munich ana alama 50 nafasi ya pili huku Leverkusen akiwa na alama 58, wamecheza michezo 22 kila timu huku zikiwa zimesalia mechi 12 kati ya 34 zinazopaswa kuchezwa.

Kwa hesabu za haraka haraka Alonso na vijana wake wanahitaji alama 29 kati ya 36 ili watangazwe kuwa mabingwa ambazo ni sawa na mechi 9.6

Bayern Munich imepoteza sasa michezo mitatu mfululizo wakipoteza mbele ya Leverkusen, Lazio na Bochum.Hali mbaya kwa Tomas Tuchel na vijana wake msimu huu.

Alonso ataweza kushikilia bomba hadi mwisho?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live