Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Michael Carrick: Bado Sijazungumza na Ralf Rangnick

Michael Carrick Mkufunzi wa Man United, Michael Carrick

Wed, 1 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muangalizi wa timu ya Manchester United Michael Carrick, amesema kuwa bado hajafanya mazungumzo na kocha wa muda Ralf Rangnick, kwa sasa akili yake iko kwenye mchezo wa alhamisi dhidi ya Arsenal.

Rangnick ameshakubaliana na klabu ya Manchester na ameshatangazwa tayari kama kocha muda kumalizia huu msimu, lakini hawezi kuwa kwenye benchi la timu kwenye mchezo huo sababu bado anashughulikia vibali vyake vya kazi.

Carrick ameingoza Man Utd kwenye mchezo dhidi ya Villarreal nakushinda 2-0 kwenye ligi ya mabingwa Ulaya, pia alioongoza kwenye mchezo wa jumapili wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Chelsea na walitoka sare ya 1-1. Pia Michael Carrick anatarajiwa kuwepo kwenye benchi kesho siku ya alhamisi kwenye mchezo dhidi ya Arsenal na utakuwa mchezo wake wa tatu kuiongoza Man Utd tokea Ole Gunnar afutwe kazi.

Rangnick ationgoza Man Utd kwenye michezo 20, kabla ya kuchukua nafasi ya kuwa mshauri wa timu kwa muda wa miaka miwili kwenye viunga vya Old Trafford.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live