Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Miamba imesepa na mabao yake

Moses Phiri X Baleke.png Miamba imesepa na mabao yake

Thu, 8 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ligi Kuu Bara imefikia patamu kwa sasa ikiwa imeingia duru la pili kwa baadhi ya timu, huku nyingine chache zikisubiri kucheza viporo kukamilisha mechi za duru la kwanza.

Mpaka kufikia sasa Yanga ikiwa kileleni na alama 34, huku ikifuatwa na Azam yenye pointi 31 na kisha Simba ikiwa na 26.

Katika mzunguko huu, ndipo ambapo kuna vita vya ubingwa kwa timu zinazopambania nafasi ya kati na zile zinazojiepusha kushuka daraja.

Lakini, wiki chache zilizopita klabu za ligi hiyo zilipata fursa ya kuboresha vikosi kupitia dirisha dogo na kuna baadhi ya nyota walijikuta wakihama na kuibukia kwingine kwenye duru hili la pili.

Kuhama sio ishu, ila ni kwamba kuna baadhi yao wamesepa na mabao yao katika klabu walizokuwa wakizichezea duru la kwanza.

Mwanaspoti inakuletea orodha fupi ya nyota waliohama na mabao  kutoka timu moja hadi nyingine, baadhi wakitimka kabisa kwenye Ligi Kuu Bara kama utani vile.

JEAN BALEKE Mshambuliaji huyo Mkongomani amecheza Simba kwa msimu mmoja baada ya kusajiliwa mwa mkopo katika dirisha dogo la usajili akitokea TP Mazembe.

Amemalizana na timu hiyo na kutimkia Al Ittihad ya Libya kwa mkopo wa mwaka mmoja, akiondoka Simba akiwa ameifungia mabao sita msimu huu.

MOSES PHIRI Mshambuliaji wa Zambia, Moses Phiri ametolewa kwa mkopo katika timu ya Power Dynamos baada ya kushindwa kuonyesha maufundi aliyoyaonyesha msimu wake wa kwanza ndani ya Simba.

Wekundu wa Msimbazi wamefanya uamuzi wa kumtoa kwa mkopo akiwa tayari ameifungia timu hiyo mabao matatu msimu huu ambayo aliyafunga dhidi ya Dodoma Jiji, Singida Fountain Gate na Ihefu FC.

MAROUF TCHAKEI Huyu ni kiungo mshambuliaji wa zamani wa Singida Fountain Gate aliyetimkia zake Ihefu FC katika dirisha dogo la usajili baada ya kuuzwa na matajiri wa kulima alizeti.

Tchakei ameondoka Singida akiwa ameifungia mabao matano hadi sasa na kwenye timu yake mpya hajapata nafasi ya kucheza kutokana na ratiba kuonyesha kuanza na Mtibwa Sugar ugenini Februari 12.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live