Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mhilu ana kitu anakitafuta huku

Mhilu Pict Mhilu ana kitu anakitafuta huku

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa zamani wa Simba na Yanga, Yusuph Mhilu amesema kuamua kwake kucheza Ligi ya Championship kuna maana kubwa kwani anakwenda kupata changamoto mpya na kujifunza vitu vipya katika ligi hiyo, akiwa na Geita Gold aliyoshuka nayo daraja.

Mhilu alisema hajawahi kucheza ligi hiyo, hivyo anajipanga kuhakikisha atakapoanza majukumu anafanya kazi ya kuisaidia timu hiyo kurejea Ligi Kuu Bara na kujifunza kitu juu ya ligi hiyo ya Championship.

"Natambua ligi hiyo ni ngumu, kwani nilikuwa naifuatilia, siyo vibaya kwenda kujifunza changamoto nyingine katika karia yangu, bado hatujaingia kambini kwa sasa sina budi kufanya mazoezi binafsi.

Aliongeza "Nilichogundua kwenye Ligi ya Championship, inahitaji nguvu na pumzi, vinginevyo mchezaji anayetoka Ligi Kuu anaweza akajikuta anashindwa kuonyesha kiwango chake."

Mhilu alisema msimu uliopita haukuwa mzuri, alikumbwa na changamoto za majeraha mara kwa mara, akajikuta anashindwa kuonyesha kiwango "Majeraha yalinitesa sana, ila kwa sasa naendelea vizuri, nipo tayari kwa majukumu."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live