Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mhilu: Tunaanza na Azam

Mhilu Sugar Mhilu: Tunaanza na Azam

Wed, 20 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kesho Kagera Sugar ina kibarua  cha kuizuia Azam FC iliyo kwenye fomu katika Ligi Kuu Bara, lakini beki wa pembeni wa timu hiyo, Dickson Mhilu amesema matajiri hao waje tu itafahamika hukohuko uwanjani.

Kagera imetoka kupoteza kwa mabao 3-0 mbele ya Simba na kesho itaikaribisha Azam inayoongoza msimamo wa ligi hiyo kwa pointi 28, kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba kuanzia saa 1:00 Usiku. Timu hiyo ina kibarua kizito Desemba baada ya kesho, inaikaribisha Yanga.

Mhilu ambaye aliwahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa Ligi Kuu, alisema ratiba hiyo ni ngumu lakini watapambana kuhakikisha wanavuna alama tatu nyumbani dhidi ya Azam kisha wasuke mipango ya kuisimamisha Yanga.

“Ratiba ni ngumu sana, pia tukimalizana na Azam wanakuja Yanga, tutapambana, tupo kwenye maandalizi, mwalimu anajazia palipo pungua ili tupate chochote kwenye hiyo michezo,” alisema Mhilu anayemudu nafasi ya beki na winga wa kulia.

Kiungo wa timu hiyo, Ally Ramadhan ‘Kagawa’, alisema kiwango bora walicho nacho Azam hakipaswi kubezwa, hivyo kikosi chao kimefanya maandalizi ya kutosha yatakayowahakikishia ushindi au matokeo chanya huku akiwaomba mashabiki kufika kwa wingi kuwapa nguvu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live