Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mhesa aitosa Mashujaa FC

Mhesa Aitosa Mhesa aitosa Mashujaa FC

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Zikiwa zimebaki siku tano dirisha la usajili wa wachezaji kufungwa nchini, kiungo mshambuliaji wa Mashujaa FC, Ismail Aidan Mhesa amevunja mkataba na baada ya makubaliano ya pande mbili.

Kiungo huyo aliyewahi kupita Mtibwa Sugar, alijiunga na Mashujaa FC mwanzoni mwa msimu huu wakati wa dirisha kubwa la usajili, lakini mambo hayajaenda vizuri hivyo ameachana nayo.

Kwa mujibu wa meneja wake, Mohammed Mshangama tayari wamepokea ofa nyingi zikimtaka kiungo huyo.

"Ni kweli amevunja mkataba na timu hiyo. Sasa tunaangalia ofa zilizopo mezani ni ipi itakuwa na manufaa kwa mchezaji ili kuweza kumalizana nayo," amesema meneja huyo.

"Sababu za kwanini mchezaji wangu ameamua kuvunja mkataba tunaomba ibaki kuwa siri ya mwajili na mchezaji, kikubwa ni kwamba Mhesa ni mchezaji huru kama kuna timu inahitaji huduma yake ije tukae mezani kwa ajili ya mazungumzo."

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: