Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgunda ndiyo kocha bora msimu huu - Ahmed Ally

Juma Mgunda   .jpeg Juma Mgunda.

Fri, 10 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja Habari na Mawasilino wa Klabu ya Simba SC, Ahmed Ally amesema kuwa Kaimu Kocha Mkuu wa Timu hiyo, Juma Mgunda ndiye kocha bora wa msimu huu.

"Kwa kweli Juma Mgunda ni Kocha mzuri sana, hebu fikiria unamkabidhi timu kocha huyu akiwa na mshambuliaji tegemeo kutokea pembeni kama Chasambi, Balua na akiwa na beki wa pembeni kama Israel Mwenda, bado amefanya kazi na hawa watu na Simba SC inapata matokeo mazuri, unadhani nini ni kimeleta hii kitu? Ni ubora aliokuwa nao Mgunda.

"Kwanza ameshatwaa Ubingwa kwenye Ligi Kuu ya Wanawake, taarifa sijui mnazo? Jana tumeshinda mabao manne, huyu ni Kocha Bora sana, kwa sababu ndani ya msimu mmoja amefundisha timu mbili tofauti na zote amezipa mafanikio, ameipa Ubingwa Simba Queens, amekuja Simba Senior Team, Simba SC inaelekea kupigania nafasi mbili za juu na zenye thamani kwenye Ligi yetu. Kwani asiwe Kocha Bora?

"Waambieni watu Juma Mgunda ndio Kocha Bora msimu huu, kama unabisha mchukuwe Kocha wako, mpe timu ya wanawake kama anaweza kuchukuwa Ubingwa, maana yake huyu mtu ana maarifa mengi sawa na akina Isaac Newton.

"Kusema ukweli anashawishi kumkabidhi jahazi aliendeshe, kwa sababu anaweza na amethibitisha hilo, hii Simba SC ilivyokuwa hohe hahe, Juma Mgunda ameirudisha katika ubora wake, hivi nyinyi hamshtuki? Kwa hiyo hata viongozi wa Simba SC nao watakuwa wanajiuliza nini cha kufanya kwa kocha Mgunda.

"Na Juma Mgunda hapigani na waamuzi, ukimuona Mgunda yeye anafurahi muda wote, huyu amefunzwa, sio msela msela, yeye anakukumbusha hebu chezesha kwa haki, sio kwamba hana nguvu, huyu anaheshima na anamuheshimu kila mtu,” amesema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live