Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgunda kabeba 19 ugenini

Mgunda Kocha Juma Mgunda

Sun, 25 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Sare ya bao 1-1 ya Simba ugenini dhidi ya Kagera Sugar, inaweka gepu la pointi sita baina yake na kinara wa Ligi Kuu Bara kwa pointi 44, lakini usichokijua ni kwamba chini ya Juma Mgunda, wekundu hao wamevuna jumla ya pointi 19.

Pointi hizo zinatoka na sare nne, kupoteza mchezo mmoja na kushinda mitano kati ya mechi 10 ilizocheza hadi sasa ugenini.

Japo michezo mingine ilichezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Simba ikiwa ugenini ilikuwa dhidi ya Azam ikipoteza bao 1-0, Yanga sare ya 1-1 na ile ya kuinyoosha Ruvu Shooting mabao 4-0.

Michezo ambayo Simba ilisafiri nje ya Dar ni dhidi ya Tanzania Prisons ilishinda bao 1-0, Singida Big Stars 1-1, Mbeya City 1-1, Polisi Tanzania ilishinda 3-1, Geita Gold iliipiga 5-0, Kagera Sugar 1-1 na inatarajia kucheza na KMC katika Uwanja wa Kirumba, Mwanza.

Baadhi ya mastaa ambao timu zao zimegawana pointi na Simba, walizungumzia kiwango cha mastaa wa Wanamsimbazi, kwamba kuna wachezaji wazoefu, hivyo kabla ya mchezo wanakuwa wanawasoma mbinu zao.

Beki wa Kagera Sugar, David Luhende alisema wanapokutana na timu kama Simba, Yanga na Azam FC ambazo zina wachezaji wazoefu wanajua namna ya kukabiliana nao, ili kuhakikisha hawadondoshi pointi. “Kutoka sare na Simba haina maana wana kikosi kibaya, isipokuwa lazima kujua namna ya kucheza nao, kuhakikisha hatupotezi mechi, ukitaka kumshinda mpinzani wako lazima ujue ubora na udhaifu wake,” alisema.

Winga wa SBS, Deus Kaseke ambaye aliwahi kuichezea Yanga alisema kutoka sare ya bao 1-1 Simba ni kutokana na kukutana timu zenye wachezaji wazoefu, hivyo kwa vyovyote vile mchezo lazima ungekuwa mgumu.

“Nimezungumzia uzoefu wa baada ya kukutana, lakini haina maana Simba siyo timu nzuri, bali ni ushindani wa kila timu kupambania malengo yake na huu mzunguko wa pili ndio mgumu zaidi,” alisema.

Chanzo: Mwanaspoti