Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgunda awahi kumalizana na Indonesia

Morocco Mgunda.jpeg Mgunda awahi kumalizana na Indonesia

Wed, 29 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kaimu Kocha Mkuu wa Simba na timu ya taifa 'Taifa Stars', Juma Mgunda anatarajia kuuwahi mchezo wao wa kwanza wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Indonesia unaotarajiwa kuchezwa Juni mbili mwaka huu.

Mgunda ameondoka nchini leo akiongozana na wachezaji watatu kwenda kuungana na timu ya Taifa ambayo ipo nchini Indonesia kujiandaa na mechi ya kuwania kufuzu ushiriki wa Kombe la Dunia dhidi ya Zambia.

Stars kabla ya kuvaana na Zambia, Juni 2 itacheza mechi ya kirafiki na wenyeji wao kwenye Uwanja wa Gelora Bung Karno unaoingiza mashabiki 9,170 utakaopigwa saa sita mchana kwa saa za Tanzania.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mgunda alisema ameongozana na wachezaji wake kutoka Simba ambao wameanza safari kujiunga na wenzao waliotangulia nchini humo.

"Nipo na nahodha Mohammed Husein 'Tshabalala', kipa Ally Salim na Edwin Barua tunaelekea huko tayari kwa ajili ya maandalizi ya kuwavaa Zambia kwenye mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia," amesema na kuongeza;

"Hatukupaswa kuwa na muda wa kupumzika kwa sababu mchezo upo karibu na kuna wengine wametangulia huko hivyo naamini kuongezeka kwetu tukiwasubiri wengine kutoka Azam FC na Yanga kutaongeza nguvu kikosini," amesema Mgunda.

Juni 11, mwaka huu, Taifa Stars inatarajia kucheza mchezo huo wa kundi E kwa ajili ya kufuzu Kombe la Dunia 2026, mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa nchini Zambia.

Michuano ya Kombe la Dunia 2026 inatarajiwa kufanyika katika nchi za Marekani, Canada na Mexico ambapo timu tisa kutoka Afrika ndizo zitafuzu kutoka tano za awali. Katika kufuzu kutokea Afrika yamepangwa makundi tisa na kinara wa kila kundi ndiye atafuzu.

Tayari Taifa Stars imecheza mechi mbili za kundi hilo ikianza kushinda 0-1 ugenini dhidi ya Niger Novemba 18, 2023 kwenye Uwanja wa Marrakech nchini Morocco mfungaji akiwa Charles M'Mombwa.

Mechi ya pili iliyochezwa nyumbani Stars ilifungwa mabao 2-0 na Morocco kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Novemba 21, 2023.

Timu za kundi hilo ni Morocco, Zambia, Niger, Tanzania na Congo wakati Eritrea ikitolewa kwenye mashindano huku sababu zikiwa hazijawekwa wazi.

KIKOSI CHA STARS:

KOCHA: Juma Mgunda na Hemed Suleiman

MAKIPA: Ally Salim (Simba), Aboutwaleeb Mshery (Yanga), Kwesi Kawawa (Syrianska FC, Sweden) na Yona Geofrey (Tanzania Prisons).

MABEKI: Haji Mnoga (Aldershot Town, Uingereza), Bakari Mwamnyeto (Yanga), Ibrahim Bacca (Yanga), Nickson Kibabage (Yanga), Mohamed Hussein (Simba), Lameck Lawi (Coastal Union), Israel Mwenda (Simba), Mukrim Issa (Ihefu), Lusajo Mwaikenda (Azam), Pascal Msindo (Azam) na Nathaniel Chilambo (Azam).

VIUNGO: Novatus Dismas (Shakhtar Donestsk, Ukraine), Yussuf Kagoma (Singida Fountain Gate), Morice Michael (RFK Novi Sad, Serbia), Himid Mao (Tala'ea El Gaish, Misri), Feisal Salum (Azam), Mudathir Yahya (Yanga), Yahya Zayd (Azam) na Abel Josiah (TDS - TFF Academy)

WASHAMBULIAJI: Edwin Balua (Simba), Saimon Msuva (Alnajmah, Saudi Arabia), Kibu Denis (Simba), Cyprian Kachwele (Whitecaps 2, Marekani), Ben Starkie (Ilkeston Town, Uingereza), Charles M'mombwa (Macarthur, Australia), Wazir Junior (KMC), Ibrahim Hamad (Zimamoto), Kelvin John (Genk, Ubelgiji), Abdul Suleiman (Azam) na Clement Mzize (Yanga).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live