Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgunda atua Mashujaa FC

Ismail Mgunda Mz Mgunda atua Mashujaa FC

Mon, 15 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Mashujaa imetangaza kuwasajili straika Ismail Mgunda kutoka Singida Black Stars na kiungo mshambuliaji kutoka Kagera Sugar, Ally Nassor 'Ufudu' kwa ajili ya kuboresha kikosi chao kuelekea Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Taarifa iliyotolewa jana na Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo imesema mbali na wachezaji hao, pia imesajili wachezaji wawili kutoka KenGold, beki wa kulia kutoka KenGold, Robert Mathias na kiungo mshambuliaji, Yusuph Dunia.

"Tumesajili wachezaji watatu wapya, Mgunda kutoka Singida, ambaye ni mshambuliaji, atakitumikia kikosi chetu msimu ujao wa mashindano, tumempata 'mbavu ya kulia', Robert 'Makidala' akitokea KenGold na kiungo wa 'boli', Ufudu, na wenzake Dunia kutoka KenGold," ilisema taarifa ya Mashujaa FC.

Mashujaa FC yenye maskani yake Kigoma, ambayo ilianza kucheza Ligi Kuu msimu uliopita imeanza kwa usajili huo, baada ya kuondokewa na wachezaji watatu ambao ni Adam Adam aliyetimkia Azam FC, Omari Omari, aliyejiunga na Simba na Reliants Lusajo, ambaye taarifa zinasema huenda akatangazwa kwenye kikosi cha Dodoma Jiji FC hivi karibuni.

Aidha, kikosi hicho kinatarajia kuondoka Kigoma kwenda kupiga kambi mjini Zanzibar kwa ajili ya matayarisho ya mashindano msimu ujao ambayo ni Ligi Kuu Tanzania na Kombe la Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), maarufu Kombe la FA.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live