Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgunda anahitajika kwenye soka la wanaume

Mgunda X Simba Queens Mgunda anahitajika kwenye soka la wanaume

Tue, 27 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya michezo nchini kupitia runinga ya TV3, Boiboi Mkali amesema kuwa Kocha wa Timu ya wanawake ya Simba maarufu kama Simba Queens, Juma Mgunda bado anahitajika kwenye soka la wanaume.

Boiboi amesema hayo kutokana na uwezo mkubwa ambao kocha huyo amekuwa akiuonesha kwenye Kikosi cha Simba SC ya wanaume kabla ya kupelekwa Simba Queens mara kadhaa ambako nako amekuwa akifanya makubwa.

Simba Queens chini ya Kocha Mgunda wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa misimu kadhaa ikiwemo msimu uliopita.

Mabingwa wa ligi ya wanawake ya Kenya, Kenya Police Bullet FC wamewatoa Simba Queens ya Tanzania kwenye hatua ya nusu fainali ya kufuzu michuano ya Klabu Bingwa Afrika ukanda wa CECAFA.

"Nadhani Kocha Mgunda anahitajika zaidi kwenye soka la wanaume, sijaona ushindani mkubwa kwenye soka la wanawake ambao unapelekea Mgunda kufundisha soka la wanawake.

Nafikiri Mgunda angeendelea kutoa mchango wake kwenye soka la wanaume kwasababu bado Kuna kitu kikubwa anacho angeweza kuwapatia Simba," amesema Boiboi Mkali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live