Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgunda akiri ngoma ngumu CCM Kirumba

Mgunda Pic Tanga Kocha Mgunda

Sat, 17 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda amekiri kuwa Desemba 18 timu hiyo ina kibarua kigumu dhidi ya Geita Gold ingawa kikosi chake kipo tayari kwa mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na vyombo vya habari Mgunda amesema ugumu wa mchezo huo unatokana na ubora wa kikosi cha Geita ambacho kimesheheni wachezaji wenye vipaji.

“Ni mchezo mgumu kwa kweli ila lengo letu kama Simba ni kuchukua pointi zote tatu,” amesema Mgunda.

Kocha huyo amesema wachezaji wake wana ari ya juu kuelekea mchezo huo utakaochezwa kwenye dimba la CCM Kirumba, Mwanza.

Amesepa pamoja na lengo la ushindi pia watacheza kwa tahadhari kwani Geita ina safu nzuri ya ushambuliaji inayoongozwa na mkongwe Saido Ntibazonkiza na Nahodha Dany Lyanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live