Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgunda ainyooshea kidole safu ya ushambuliaji Simba SC

Mgunda Kocha Juma Mgunda

Sun, 30 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa kikosi cha Simba, Juma Mgunda amepeleka lawama zake kwa mastraika wa timu hiyo kutokana na kushindwa kuzitumia nafasi walizopata.

Simba walipoteza mchezo wa ligi dhidi ya Azam juzi alhamis kwenye Uwanja wa Mkapa, kwa bao 1-0 likifungwa na Prince Dube.

Akizungumzia matokeo hayo Mgunda alisema: “Kwanza namshukuru Mungu mchezo umemalizika salama, tumejitahidi kwa ajili ya kuhakikisha tunashinda mchezo lakini imeshindikana.

“Mchezo ulikuwa mzuri tumetengeneza nafasi nyingi za wazi lakini tumeshindwa kuzitumia, wenzetu wametengeneza nafasi na wameitumia hivyo ndivyo mpira wa miguu ulivyo.

“Tunarejea mazoezini kwa ajili ya kurekebisha hayo makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo uliopita ili leo dhidi ya Mtibwa yasijirudie tena.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live