Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgunda aibuka na haya kwa wachezaji wa Simba

Newslite1666517491860 Mgunda Kocha Mgunda

Mon, 24 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Simba SC Juma Mgunda, amesema wachezaji walipambana wakati wote wa mchezo dhidi ya watani wao Yanga lakini hatukufanikiwa kupata alama tatu.

Mgunda amesema wachezaji walicheza vizuri na walijitoa mpaka tone la mwisho la jasho lakini siku zote mpira una matokeo matatu, ambapo wamepata alama moja hivyo watajipanga kwa mchezo ujao.

Mgunda ameongeza kuwa mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo wa leo atayafanyia kazi mazoezini na mazuri atayaboresha ili mechi ijayo apate alama tatu.

“Wachezaji wamepambana muda wote, lengo lilikuwa ni kupata pointi tatu lakini haikuwa hivyo. Tuliingia kwa kujua utakuwa mchezo mgumu na tulijitahidi kuwadhibiti wapinzani.

“Katika mchezo wa leo (jana) kulikuwa na mazuri ambayo tutayaboresha ili tufanye vizuri mechi inayofuata na yale mapungufu tutayafanyia kazi mazoezini,” amesema Mgunda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live